Mahakama kuu ya DSM imeanza kusilikiza kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na kada wa CHADEMA

Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imeanza kusilikiza kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na kada wa Chadema ili kutoa uamuzi wa kwamba wananchi wanatakiwa kukaa mita ngapi baada ya kupiga kura ambapo kwa kuanza  imeshauri mlalamikaji kubadilisha madai yake badala ya kumshtaki mwenyekiti wa tume ya uchaguzi imshtaki mkurugenzi wa tume hiyo kwa sababu yeye ndio mtendaji mkuu na siyo mwenyekiti.

Kesi hiyo ambayo inasikilizwa na jopo na majaji watatu wakiongozwa na jaji Sakieti Kihiyo limeshauri upande wa walalamikaji kuwa kutokana ana mwenyekiti wa tume kutokuwa na mtendahi mkuu wa tume ni vyema wafanye mabadilki kabla shauri hilo halijaanza kusikilizwa kwa kina ili kuepuesha uiwezekano wa upande wa serikali kuweka pingamizi kuwa aliyeshtakiwa siyo muhuska.

Kutokana na ushauri huo wakili Peter Kibatala ambaye anamtetea mteja wake Bw Amy Kibatala ambaye ni mgombea ubunge viti maalum jimbo la Kilombero aliridhia kubadilisha hati ya mashtaka na sasa wanamshtaki mwanasheria mkuu wa serikali na mkurugenzi wa tume ya uchaguzi.
 
Shauri hilo linatarajiwa kuanza kusikilizwa rasmi tarehe 21 mwezi huu baada ya wakili wa serikali mkuu Obadia Kameya kudai mahakamani hapo kuwa  hawajapaa muda wa kutosha kujibu hoja za upande wa pili na hivyo wanaomba kuwasilisha majibu yao ili kutoa fursa ya kesi kuanza kusilizwa.
 
Msingi wa madai hayo ni kwamba Amy anaiomba mahakama itoe tafsiri ya kifungu namba 104 (1) cha sheria ya uchaguzi sura 343 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010 kuwa ni umbali ganai watu wanatakiwa kukaa kutoka kwenye kituo cha kupigia kura.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo