Magufuli achekelea baada ya kuhisi "kuionja" Ikulu

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amezidi kukaribia lango la Ikulu kutimiza ndoto yake ya kuwa mrithi wa Rais Jakaya Kikwete katika serikali ya awamu ya tano, baada ya kuzoa maelfu ya kura na kuongoza katika majimbo 156 kati ya 195 yaliyotangazwa hadi kufikia jana jioni.
 
Katika matokeo hayo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili iliyopita na kuanza kutolewa juzi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Dk. Magufuli amemuacha mbali mpinzani wake wa karibu katika kinyng’anyiro hicho, Edward Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). 
 
Kwa mujibu wa matokeo hayo, Lowassa anaongoza katika majimbo 39 kati ya hayo (195) yaliyotangazwa hadi kufikia jana jioni. 
 
Kwa ujumla, idadi ya kura zilizovunwa na Dk. Magufuli katika majimbo hayo 195 kati ya yote 264 ni 6,026,197, huku mpinzani wake Lowassa anayewakilisha pia muungano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya NLD, NCCR-Mageuzi na Chama cha Wananchi (CUF), akipata kura 4, 251, 282.
 
Kwa hesabu hizo, maana yake ni kuwa tayari Magufuli amemzidi Lowassa kwa idadi ya kura 1, 774,915,  hivyo kujisafishia njia ya kuwa mshindi na mwishowe kutinga Ikulu.
 
Mbali na Magufuli na Lowassa, wagombea wengine wa urais wameachwa mbali zaidi kwani hadi kufikia jana, idadi ya kura walizopata kwa pamoja hazijawahi kuvuka 10,000. Wagombea hao walio nyuma ya Magufuli na Lowassa ni Hashim Rungwe wa Chaumma, Janken Kasambala (NRA), Fahmy Dovutwa (UPDP), Anna Mghwira (ACT-Wazalendo), Chifu Lutasola Yemba (ADC) na Maximillian Lyimo wa TLP.
 
MATOKEO KATIKA MAJIMBO 82
Jana, Mwenyekiti wa Nec, Jaji mstaafu Damian Lubuva, alitangaza matokeo ya majimbo 82, huku 51 yakitangazwa hadi kufikia mchana na mengine 31 jioni. Magufuli wa CCM alikuwa akifanya vizuri kwa kupata kura nyingi zaidi dhidi ya Lowassa wa Chadema.
 
Katika Jimbo la Tanga Mjini, CCM ilipata kura 65,340 huku Chadema ikipata kura 56,939.
 
Jimbo la Lupa, CCM 37,684, Chadema 20,175; Lushoto, CCM 28,058, Chadema 8,673; Rorya, CCM 54,892, Chadema 36,569; Musoma Mjini; CCM 33,658, Chadema 25,352.
Jimbo la Mvomero CCM 68,179, Chadema 33,468; Hai CCM 29,341, Chadema 49,125; Bukombe CCM 50,063, Chadema 28,106; Bagamoyo CCM 29,697, Chadema 16,245.
 
Iringa Mjini CCM 36,584, Chadema 38,860; Sumbawanga CCM 43,542, Chadema 34,201; Same Mashariki CCM 18,520, Chadema 17,874; Sengerema CCM 69,392, Chadema 28,335.
 
Jimbo la Moshi Vijijini CCM 25,017,  Chadema 54, 823; Bukoba Vijijini CCM 27,620, Chadema  25,898; Kilosa CCM 55,839, Chadema 24,276; Mikumi CCM 35,192, Chadema 26,84.
 
Jimbo la Mlimba CCM 39,555, Chadema 35,994; Kasulu Mjini
CCM 32,297, Chadema 15,762; Mbogwe, CCM 44,558, Chadema 12,040; Shinyanga Mjini CCM 41,692, Chadema 25,465.
 
Jimbo la Ushetu, Shinyanga CCM 51,034, Chadema 21,585; Busanda, CCM 73,834, Chadema 35,373; Mtwara Vijijini CCM 25,938, Chadema 24,518.
 
Jimbo la Tarime Mjini CCM 18, 009, Chadema 15,992; Ludewa CCM 35,364, Chadema 11,715; Msalala, Shinyanga CCM 44,215, Chadema 16,942; Kishapu CCM 65,173, Chadema 17,177; Mlalo CCM 33,996, Chadema 8,938; Kahama Mjini CCM 58,728, Chadema 27,501; Rombo CCM 21,908, Chadema 57,715.
 
Jimbo la Kalenga, Iringa CCM 40,896, Chadema16,890; Mpanda Mjini CCM 32,770, Chadema 16,599; Kavuu CCM 21,483, Chadema 8,083; Ismani CCM 26,766, Chadema 15,303; Nyasa CCM 30,609, Chadema 14,062.
 
Jimbo la Mufindi Kaskazini, CCM 26,412, Chadema 8,085; 
Tunduma CCM 19,446, Chadema 32, 219; Jimbo la Liwale
CCM 19, 967, Chadema 23,176; Jimbo la Gairo CCM 44,656 9, Chadema 6,925; Kilolo CCM 52,517, Chadema 25,424.
 
Jimbo la Busega, CCM 47,049, Chadema 19,765; Kalambo CCM 38,165, Chadema 29,501; Sumve CCM 32,079, Chadema 11,203; Mbinga Vijijini CCM 55,855, Chadema 12,213;  Kilombero CCM 49,478, Chadema 49,166; Bahi CCM 51,138, Chadema 11,340; Chato CCM 83,820, Chadema 27,936.
 
Jimbo la Geita CCM 45,472, Chadema 18,640; Magu CCM 69,961, Chadema 30,070 ; Kwimba CCM 40,544, Chadema 10,071.
 
Jimbo la Segerea, CCM 99,168, Chadema 119,356; Geita Mjini, CCM 43,576, Chadema 25,030; Rufiji, CCM 21,714, Chadema 18,308; 
Kibiti, CCM 21,142, Chadema 18,629.
 
Katika Jimbo la Mbarali, CCM kura 55,933, Chadema 45,374; Bariadi, CCM 85,813, Chadema kura 57,922; Temeke, CCM 106,612,  Chadema 124,276;  Ubungo, CCM 71,928, Chadema 83,637.
 
Katika Jimbo la Busokelo, CCM 18,834, Chadema 12,596; Kwera, CCM 49,196, Chadema 32,980; Morogoro Kusini, CCM 35,505, Chadema 13,586; Karagwe, CCM 62,159, Chadema 41,676; Muheza, CCM 53,237, Chadema 22,635.
 
Katika Jimbo la Ilala CCM 37,329,  Chadema 36,330; Bububu, CCM 10,026, Chadema 7,332; Tabora Mjini, CCM 52,909, Chadema  30,027; Arumeru Mashariki, CCM 31,040, Chadema 88,912; Nyamagana, CCM 99,890, Chadema 78,329.
 
Mtwara Mjini, CCM 25,828, Chadema 30,155; Bukoba Vijijini, CCM 64,839, Chadema 32,346; Songwe, CCM 30,778, Chadema 14,738; Chemba, CCM 51,594, Chadema 20,800; Buchosa, CCM 62,762, Chadema 31,660.
Katika Jimbo la Kilwa Kaskazini, CCM 17,553, Chadema 14,722.
 
Kibakwe, CCM 36,830, Chadema 8,018; Kilwa Kusini, CCM 18,767, Chadema 22,377; Morogoro Kusini Mashariki, CCM 30,624, Chadema 13,304; Hanang, CCM 63,205, Chadema 32,367; Morogoro Mjini, CCM 85,440, Chadema 65,580 na Kigamboni, CCM 35,735, Chadema 39,754.

Chanzo:Nipashe


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo