Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema,
Edward Lowassa jana alitua kwa mara ya kwanza kwenye Jimbo
la Karatu ambako Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
alitumia nafasi hiyo kuwaeleza wananchi sababu za kumuacha
Dk Willibrod Slaa kugombea urais na badala yake kumteua Dk Willibrod Slaa kugombea urais na badala yake kumteua
waziri huyo mkuu wa zamani.
Lowassa pia alivuta watu wengi kwenye mkutano uliofanyika
Uwanja wa Mashujaa mjini Moshi, ambako Jaji Salma Maghembe alilazimika kuahirisha kwa
muda kutoa uamuzi wa ubishani wa kisheria katika kesi ya mauaji ya bilionea maarufu, Erasto Msuya kutokana na kelele zilizosababishwa na honi za pikipiki, vuvuzela na nyimbo.
Mahakama
hiyo inapakana na Uwanja wa Mashujaa.
Kwenye mkutano wa kampeni za urais uliofanyika Karatu, Mbowe alilazimika kuzungumzia suala
la Dk Slaa, ambaye alijivua wadhifa wake akipingana na viongozi wenzake katika taratibu za
kumpokea Lowassa kutoka CCM na kumpa fursa ya kugombea urais.
Akizungumza kabla ya kumpisha Lowassa ahutubie, Mbowe alisema malengo ya nchi ni makubwa
kuliko Dk Slaa na Lowassa.
Alisema Chadema iko tayari kumsamehe Dk Slaa kwa kuwa kila mtu kuna wakati hufanya makosa
ambayo ni vitu vinavyosameheka.
“Nasikitika kwamba tumepoteza askari mmoja, lakini mapambano ya kuikomboa nchi
yanaendelea,” alisema Mbowe ambaye alikuwa akizungumza kwa mara ya kwanza na wananchi wa
Karatu tangu Dk Slaa alipojiondoa Chadema mapema mwezi uliopita.
“Mwaka 2010 niliombwa kugombea urais, lakini nilimshawishi Dk Slaa agombee akaniuliza,
“mwenyekiti nitaweza?” Nikamjibu, “utaweza”, kwa kuwa nilimpima na alikuwa na sifa na uwezo
wa kuwa rais,” alisema Mbowe.
“Mwaka huohuo, rafiki yangu alianza mahusiano ya kifamilia. Dokta wetu akawa siyo yule
tuliyemzoea. Ilipofika mwaka 2014 akaniambia niwe mgombea, lakini nikamwambia bado anafaa
hivyo nikapeleka mapendekezo kwenye vikao vya chama wakaniambia, ‘mwenyekiti kwa nini
unaleta mapendekezo?’ Nikawaambia ndani ya Chadema hatugombanii uongozi.
“Tulimpendekeza Dk Slaa agombee urais. Chama hiki tumekijenga kisayansi tukafanya utafiti kwa
kutumia watafiti kutoka nje ambao hawamjui Lowassa. Mbowe wala Slaa.
Maswali yetu yalikuwa
manne; la kwanza nini matumaini ya Chadema kukamata nchi chini ya Dk Slaa? Nani miongoni
mwa wanaCCM anaweza kuongoza mabadiliko? Tufanye nini ili safari yetu iwe ya uhakika?
Lakini majibu hayakuwa mazuri.”
Alisema watafiti hao waliwaambia Chadema ina nguvu lakini ifanye jitihada iipasue CCM ili iweze
kufika na iliwaeleza kuwa atakayekisumbua chama hicho kikuu cha upinzani ni Lowassa kwa
kuwa ana kundi kubwa ndani na nje ya CCM.