Wazee CHADEMA wasema Kuhama kwa Kingunge kusiwe sababu ya kumkebehi

Baraza la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA limekemea tabia ya kukebehi na kudhihaki kitendo alichokifanya kada mkongwe wa CCM Kingunge Ngombale Mwiru cha kukihama Chama hicho na kudai kuwa kila Mtanzania ana uhuru wa kujiamulia masuala yake binafsi.

Wamedai kuhama chama kusipokelewe kama dhambi bali ni ukomavu wa mtu katika demokrasia.

Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Chadema Rodriki Rutembeka anazungumza na waandishi kuhusu hali halisi inavyoendelea tangu Mzee Kingunge afanye uamuzi wa kukihama chama chake kilichomlea na kudai kuwa wapo watu ambo wanatumia fursa hiyo kumkashifu kama vile hana haki ya kufanya hivyo na kuwataka watu hao kuacha mara moja.

Mwenyeki wa wadhamini wa Chadema, Alcardo Ntagazwa amedai ubabe uliopo ndani ya viongozi wa CCM ni chanzo cha kuzorotesha maendeleo ya nchi japokuwa nchi inazo rasilimali nyingi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo