Tume ya Uchaguzi Zanzibar imeufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar kutokana na kuwa na dosari nyingi ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru na wahaki
Mwenyekiti wa ZEC ametoa tangazo hilo kupitia shirika la utangazaji la ZBC mchana huu kuwa amechukua maamuzi hayo baada ya kujiridhisha kuwa uchaguzi uligubikwa na dosari nyingi.
"Mimi nikiwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, nimeridhika kuwa Uchaguzi huu umegubikwa na makosa makubwa....
"Kwa mamlaka niliyonayo natangaza rasmi kuufuta uchaguzi huu kwa kuwa haukuwa huru na wa haki, mtajuulishwa tarehe itakayofanyika uchaguzi mwengine hapo baadae, Ahsanteni kwa kunisikiliza"! - Jecha S. Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).