Mwanaume ambaye hajafahamika jina lake, amefika kwenye
kituo cha kupiga kura cha Mtoni Kijichi A, kisha akaanza
kuhubiri kwa sauti kubwa akimwomba Mungu awabariki wapiga
kura.
Wakati akiendelea kuhubiri alikuwa akielekea kwenye chumba
cha kupigia kura.
"Mungu awabariki mpige kura kwa amani, mbarikiwe, jamani mnanisikia?" Alisema.
Hata hivyo mtu huyo aliyekuwa akizungumza huku akipepesuka, alizuiwa kuingia kupiga kura na
askari aliyekuwa mlangoni kwa madai kuwa hakuwa amefuata taratibu.
Baada ya askari kuzungumza nae alitaka aruhusiwe kuingia kupiga kura, lakini baadhi ya
wananchi walipinga wakisema mtu Hugo ni mlevi.
"Kalewa huyo tunamjua akapange mstari kule nyuma," alisema mmoja wa wapiga kura.