Kwa ufupi, Walioandikishwa kupiga kura ni 48,379, idadi ya kura zilizokataliwa 645, kura halali 37,063, kura halisi 37,063, Joma Amos Mwakisitu wa ACT Wazalendo amepata kura 430, Jackson Taifa Mbogela wa CHADEMA amepata kura 15,022 na Norman Adamson Sigalla King wa CCM amepata kura 21,611.
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Makete ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Francis Namaumbo (aliyesimama) akitangaza matokeo ya Ubunge jimbo la Makete jana jioni katika ukumbi wa halmashauri hiyo
Mshindi wa Ubunge jimbo la Makete kupitia CCM Prof Norman Sigalla akipokea cheti cha kuonesha kuwa ndiye aliyeibuka kidedea katika uchaguzi huo kutoka kwa msimamizi wa Uchaguzi Bw Francis Namaumbo
Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Makete kupitia CHADEMA Jackson Mbogela Taifa akipeana mkono na Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Makete mara baada ya matokeo kutangazwa
Katibu wa CCM wilaya ya Makete akimpongeza mbunge mteule wa jimbo la Makete Prof Norman Sigalla baada ya kutangazwa mshindi
Mbunge mteule wa jimbo la Makete kupitia CCM Prof Norman Sigalla akizungumza baada ya kutangazwa kuwa ni mshindi
Wananchi wakifuatilia zoezi la kutangaza matokeo jimbo la Makete
Wakisikiliza kwa makini zoezi la kutangaza matokeo hayo
Jackson Mbogela aliyekuwa mgombea ubunge Makete kupitia CHADEMA akifuatilia zoezi la kutangaza matokeo
Prof Norman Sigalla akipiga makofi baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha Ubunge jimbo la Makete kupitia CCM
Joma Mwakisitu aliyekuwa akigombea ubunge Makete kupitia ACT - Wazalendo akifuatilia zoezi la kutangazwa matokeo hayo
Haya ndiyo matokeo ya uchaguzi jimbo la Makete. Na Edwin Moshi wa Eddy Blog, Makete