Jeshi la Polisi mkoani Geita linamtafuta aliyekua
mgombea wa ubunge kupitia chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Rogers Ruhega kwa tuhuma za
kuhusika na shambulio la kudhuru mwili wa Moshi Paul akiwa
na vijana wengine 25.
Pia jeshi la polisi linayashikilia magari matatu yaliyokuwa
yakitumiwa na mgombea huyo kwenye kampeni kwa tuhuma za
kukutwa yakiwa na silaha mbalimbali kama mapanga,sime na
fimbo kinyume cha sheria.
Kamanda wa polisi mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo alikiri kukamatwa kwa magari hayo na
kusema yalikamatwa yakiwa na silaha hizo usiku wa kuamkia oktoba 25 majira ya saa sita usiku kulilalamikia jeshi la polisi kufika nyumbani kwake usiku wakiwa na silaha na kuitisha familia
Kamanda Mwabulambo alisema polisi wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria.
“polisi kufika nyumbani kwake ni kwa mujibu wa sheria na kama yeye ni mtu mzuri ajiulize kwa
nini polisi wafike nyumbani kwake usiku ni vyema akajisalimisha mwenyewe badala ya kusubiri
kukamatwa na polisi”alisema Kamanada.
Alisema Rogers anahusishwa na tukio la shambulio na kukutwa na silaha kinyume cha sheria na
kumtaka kujisalimisha polisi badala ya familia yake kulalamika kwenye vyombo vya habari
Awali mke wa aliyekuwa mgombea akizungumza na waandishi wa habari alidai kundi la askari
zaidi ya saba wa jeshi la polisi wamekuwa wakifika nyumbani kwake usiku wa manane wakiwa na
silaha amilia yake.
“mimi nashindwa kuwaelewa hawa polisi kwa sababu siku hawa vijana wanakamatwa hata mume
wangu alikuwepo sijui kwa nini waliwakamata hao vijana wakamuacha yeye alafu sasa ndio
wanasumbua “
Mwanamke huyo alidai kitendo kilichofanywa na polisi kukamata magari ya mume wake na
kumzuia kupeleka barua za mawakala ni sababu moja wapo iliyochangia mume wake kushindwa
katika kinyanganyiro cha ubunge katika jimbo la Geita mjini.
Katika uchaguzi uliofanyika oktoba 25 mwaka huu katika jimbo la Geita mjini ilihusisha
wagombea watatu katika nafasi ya ubunge ambapo Kanyasu John aliibuka mshindi kwa kupata
kura 34,953 sawa na 55% Rogers Ruhega alipata kura 26,303 sawa na 41.5 % na Malebo Michael
alipata kura 625 sawa na 0.1%