Akihojiwa na redio station ya voice of america mh. Tundu Lissu anasema ameshangaa sana maneno aliyoyasema leo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.
Anasema Dr.Slaa alikwisha kuteuliwa kuwa mgombea urais mwezi January na mwezi Aprili akathibitishwa na kamati kuu
Anaendelea kusema ameshangaa Dr.Slaa kusema Gwajima ndio alimleta Lowassa jambo ambalo siyo kweli kabisa, yeye Dr. Slaa mwezi wa tano ndio alianza kumtafuta Lowassa kwa kumtumia Gwajima
Anasema wakati Lowassa anapokelewa tarehe 27 July kwenye Kamati Kuu, Dr.Slaa hakulala nyumbani aliporudi nyumbani mchumba wake alimtupia mabegi nje na DR. alilala kwenye gari.
Anasema Dr. Slaa asiwadanganye watanzania tatizo ni urais na mchumba wake.