Vyombo vya Ulinzi na Usalama leo vimemwaga rasmi Amiri jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dk Jakaya Kikwete , baada ya kuviongoza vyombo hivyo kwa miaka kumi sasa.
Sherehe za Kumuaga amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama zilifanyika leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ambapo rais Kikwete aliingia uwanjani hapo kwa gari la wazi sambamba na kukagua gwaride maalum huku wimbo wa taifa na mizinga 21 ikipigwa.
Gwaride maalum lililoundwa na vikosi vya Jesh la Wananchi, JKT, Polis na Magereza vilipita mbele ya rais huku kivutio kikubwa kikiwa ni onesho la makomandoo.
Vikosi hivyo viliandaa maonesho mbalimbali ya kuonesha umahiri wao sambamba na nyimbo maalum za kumwaga kiongozi huyo .
Miongoni mwa watu waliohudhuria sherehe hizo za kumuaga ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal na viongozi wengine wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.