Saa chache baada ya wimbo mpya wa Roma ‘Viva Roma viva’ kutoka September 9, rapper huyo amedai kuwa
ametishiwa wimbo huo kufungiwa.
Kupitia Instagram, majira ya saa mbili usiku Roma aliandika;
“WANATAKA KUIFUNGIA NYIMBO YANGU!! KISA TU NIMEONGEA UKWELI!! INANIUMA SANA NATAMANI
HATA KULIA NIKIONA UKWELI HAUPEWI NAFASI!! NIOMBEENI NA MNIKUMBUKE KWENYE SALA ZENU NDUGU ZANGU!! Viva Roma viva”
Bado haijafahamika sababu ya wimbo huo kutaka kufungiwa, na Roma hakupatikana kwenye simu yake
nilipomtafuta kwaajili ya kuzungumza nae kuhusu swala hilo.
Usikilize hapa kama bado hujausikiliza