Rais Kikwete awajulia hali majeruhi baada ya mkutano wa Dkt Magufuli

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika msongamano mkubwa uliotokea katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni wa CCM katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015. Watu wawili walipoteza maisha, akiwemo mvulana wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah na mwanamama Grace George (42), ambapo jumla ya watu 17 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini hapo. Hadi jioni hii majeruhi saba walikuwa wameruhusiwa
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Samson Tarimo alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mweka Hazina wa CCM mkoa wa Morogoro Ndg. Hassan BAntu alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.
 Mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo
 Rais Kikwete akimpa pole  mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo