Ofisi za bodi ya mikopo ya elimu ya juu Zanzibar zavamiwa

Wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma katika vyuo vikuu  viliopo bara na Zanzibar  wamevamia Ofisi za bodi ya mikopo ya Zanzibar wakidai  posho zao ambazo hawajalipwa  kwa kipindi cha mwaka mzima  na  fedha za ada za masomo.

Tovuti hii iliwakuta wanafunzi hao wapatao 70 wamekusnayika  nje ya jengo la bodi hiyo ya mikopo wakitafakari na kutafuta mbinu za kudai malimbikizo ya fedha zao za posho ambazo ni zaidi ya mwka mzima hawaajlipwa na bodi hiyo imekuwa ikitoa ahadi hewa  kupata fedha hio na wameiomba seriklai ilivalie njuga suala hilo.
 
Hata hivyo mkurugenzi mkuu wa bodi hiyo ya mikopo ya Zanzibar Bw.Idi Khamis amekiri kuwepo kwa hali hiyo ya wafaunzi inagawa amesema tatizo kubwa linakuja kuwa wanafunzi hao wnyewe hawalipi madeni yao ambapo wanadai karibu bilioni 30 huku akiwahakikishia wanfunzi hao pamoja kuwa serikali tayari imeshandaa mpango wa kulipa ada mwaka huu wanapaswakueelewa kuwa sio bodi ndio yenye malaka ya kulipa fedha zote..
 
Bodi hiyo ya mikopo ya zanzibar  ambayo hutegemea ruzuku serikalini na fedha za urejeshaji  inahitaji shlingi bilioni 8 kwa mwaka kwaajili ya kuwalipia ada na posha wanafunzi wanaosoma  Tanzania bara katika vyuo mbali mbali na wakiwemo wanfunzi wa Zanzibar walioko  hapa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo