Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashimu Rungwe, amesema endapo chama chake kitapata ridhaa ya kuongoza nchi kitahakikisha kinawaondoa wakuu wa mikoa na wilaya, na kuanzisha serikali ya majimbo kwa lengo la kuboresha maadili ya utendaji.
Aidha amesema endapo atapata ridhaa hiyo atahakikisha anamaliza tatizo la ukosefu wa maji katika mkoa huo ikibidi kusambaza maji kwa kutumia HELKOPTA ili kuwaondolea adha wanayoipata wananchi wa maeneo hayo.
Akizungumza jana kwenye kampeni zake za kuwania urais, uliofanyika katika mikoa ya Tabora na Shinyanga kituo , Rungwe alisema wakuu wa wilaya na mikoa wamekua kero kwa wananchi kwa kuwa hawachaguliwi bali wanateuliwa na rais, na kwamba wamekuwa wakitumikia sera ya chama hicho kilicho wachagua.
Sera ya Chaumma kama tutapa ridhaa ya kuongoza Serikali ya Tanzania lazima tutawaondoa wakuu wa mikoa na wilaya, kwani ndio watu wanaochangia wananchi kutokuwa na maendeleo na kubaki na wimbi la umaskini,î alisema Rungwe na kuongeza kuwa.
Viongozi hawa wamekuwa wanafanya wanavyotaka kwa sababu wananchi hawajawaweka kwenye nafasi hizo, Sasa Chaumma itaanzisha serikali ya majimbo vyama vyote vishiriki kugombea nafasi hizo, kwa kufanya hivyo watawathamini wananchi, kwani wao ndio watakua wamewaweka madarakani na wanauwezo wa kuwaadhibu.
Kuhusu maji, mgombea huyo alisema inashangaz kuona hadi leo Tanzania kuna maeneo hayana huduma hiyo na hivyo kuwasababishia usumbufu wananchi, jambo aliloahidi kulimaliza kwa kusambaza maji katika maeneo hayo kwa njia yoyote ikibidi kutumia HelkoptaPia alizungumzia suala la kuanzisha kilimo cha kisasa, ambapo alisema atatumia teknolojia ya umwagiliaji kwa kutumia ndege, ili wananchi waweze kulima mazao mengi na kukabiliana na baa la njaa ambalo limekuwa likiwakabili kila mwaka na kutotegemea msaada kutoka nje ya nchi.
Alisema nchi inauwezo wa kufanya hivyo, na sasa ni wakati wa wananchi kufanya mabadiliko na kuiondoa Serikali ya CCM ambayo imeshindwa kufikilia jambo hilo kwa muda wote iliyotawala, na kwamba Chaumma kikipata nafasi hiyo itaonesha kuwa inaweza kubadilisha maisha ya Watanzania.
Chanzo:siasa.co.tz
