ITV wakanusha uchakachuaji wa kisiasa wanaodaiwa kuufanya

Uongozi wa ITV na Redio One unakanusha taarifa za uzushi zilizoenezwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zikimhusisha mwandishi wetu kuwa ameshiriki kuanzisha matawi bandia ya Chadema katika maeneo ya Tandale na kuwapanga vijana wa chama cha Mapinduzi kwa kuwavalisha nguo za Chadema kwa lengo la kususha bendera za Chadema na kupandisha ya CCM.

Taarifa hizo ni uzushi na zenye nia ovu ya kumdhalilisha mwandishi huyo .

ITV ni kituo makini chenye kuzingatia weledi ambacho hakiwezi kutumiwa au kukubali kutumika kufanikisha propaganda hizo.

Tunawasihi watazamaji na wasikilizaji wetu kuzipuuza na kuendelea kuwa na imani na watendaji wa kituo hiki.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo