Chama cha demokrasia na maendeleo kimetoa pikipiki 24 zenye thamani ya shs. 40mil/= kwa ajili ya makatibu wa kata zote 17 za wilaya hiyo ili kurahisisha utendaji kazi ili kuleta ufanisi katika ufuatiliaji wa mchakato wa uchaguzi.
Mwenyekiti wa chadema wa wilaya hiyo Bw.James Mushi amekabidhi pikipiki hizo kwa makatibu hao kwa niaba ya mwenyekiti wa taifa wa chama hicho na mbunge wa wilaya hai Mh.Freeman Mbowe.
Akikabidhi pikipiki hizo zikiwemo za ofisi kuu ya wilaya Bw.Mushi amesema, chama hicho hivi sasa kinajiandaa kuwa chama tawala na kuwaonya makatibu hao wasizitumie kwa ajili ya biashara ya boda boda ili wawe mfano wa matumizi sahihi ya raslimali za umma.
Wakipokea pikipiki hizo kwa niaba ya wenzao Bw.Ali Sadiki na Bi.Rosemary Kuringe wamekishukuru chama hicho kwa kutambua umuhimu vitendea kazi ambavyo vilikuwa kikwazo katika utendaji wao wa kazi za kila siku.
