Abiria waliokuwa wakisafiri na ndege ya shirika la ndege Norway, walijikuta wakipigwa bumbuwazi baada ya kugundua kuwa kuna wapenzi walikuwa ‘wakibanjuka’ ndani ya choo cha Ndege hiyo ikiwa angani.
Mtonyaji wa kali hii aliuambia mtandao wa Online daily, kuwa walitangaziwa na marubani kupitia vipaza sauti kwamba wamewanasa wapenzi hao wakiwa katikati ya dimbwi la mahaba.
Ndege hiyo ilikuwa ikitokea Paris kuelekea mjini Stokholm, ajabu ni kwamba mamlaka ya usafiri wa anga Norway imewapongeza kwa kufanya kitendo hicho walichokiita cha kishujaa.