Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Dk. Willibrod Slaa amesema anakwenda Marekani pamoja na familia yake kwa mapumziko.
Hata hivyo, taarifa zinasema Dk. Slaa amekwishandoka nchini
kuelekea Marekani pamoja na familia yake tangu jana jioni.
Huku akiwa Marekani kupumzika na kujiendelea katika kozi fupi katika tasnia ya Sheria na
Lugha, Dk. Slaa amesema nyumba yake itakuwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.
Akizungumza katika mahojiano yaliyorushwa leo asubuhi na kituo cha televisheni cha Azam, mwanasiasa huyo amesema akiwa mapumzikoni Marekani, nyumba yake itakuwa inalindwa na
Jeshi la Polisi kutokana na vitisho ambavyo amekumbana navyo tangu alipoamua kuachia ngazi
Chadema.
“Ninatishiwa maisha, ni lazima nichukue tahadhari….., ninatishiwa kupigwa mawe. Ni kweli
ninalindwa na usalama,” amesema Slaa akiwa anahojiwa na mwanahabari nguli, Tido Mhando.
Hata hivyo, Dk. Slaa ambaye ameshawahi kuwa mbunge wa Karatu mkoani Arusha amesema
anashangazwa na taarifa zinazoenea kuwa amelala katika hoteli ya kifahari ya Serena jijini Dar es
Salaam na kuhoji wakati wa uchaguzi mkuu, 2010, alilala mahali hapo lakini hakuna aliyehoji.
Kuhusu gharama alizotumia kufanya mkutano na wanahabari katika hoteli ya Serena, Dk. Slaa
amesema, alipoenda Marekani katika ziara ya kichama, alizuru majimbo 13 na hakutumia fedha za
Chadema bali marafiki zake ambao hakuwaweka bayana.
Dk. Slaa amesema licha ya kuwa ng’ambo katika kipindi hiki muhimu kwa taifa, ataendelea
kufuatilia yanayojiri nchini. Ameahidi kurudi kupiga kura muda ukifika.
Hapo chini Kuna Audio ya Mazungumzo yaliyorushwa leo na Azam Tv wakati akihojiwa na Tido Mhando
Hapo chini Kuna Audio ya Mazungumzo yaliyorushwa leo na Azam Tv wakati akihojiwa na Tido Mhando
