Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM John P Magufuli, amewataka wananchi kutokukilaumu na kukiadhibu chama hicho kwa makosa ya watendaji.
Akizungumza na mamia ya wananchi katika kampeni mjini Bunda mkoani Mara, Magufuli amewataka wananchi kumchagua ili amalize matatizo yaliyopo kwa watendaji mizigo serikalini aliyowaita Mchwa.
“Nawaomba wananchi msiiadhibu CCM kwa kuwa nimejipanga kuwamaliza mchwa Serikalini, nawaomba wanabunda msiipe CCM adhabu kama ambavyo huwezi kuchoma kitanda chenye kunguni, badala yake utachoma kunguni, acheni tuchome kunguni si kitanda” alisema Magufuli.