#TaarifaSeptemba23 Chama Cha Mapinduzi kinapenda kutoa taarifa kuhusu: Mwenendo wa Kampeni, Midahalo ya Wagombea & Utafiti wa Twaweza.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
#TaarifaSeptemba23 Kampeni za Dkt @MagufuliJP & Bi @SuluhuSamia zinaendelea vyema. Kila mmoja anafanya wastani mikutano 8 hadi 11 kila siku.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
#TaarifaSeptemba23 Kila siku wagombea wanakutana na maelfu ya wananchi mikutanoni. Tunawashukuru wananchi na makada wanaofanikisha haya.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
#TaarifaSeptemba23 Tunaridhika na mwenendo wa kampeni hadi sasa. Nusu hii ya pili tutaongeza kasi, msukumo & mbinu kufikia watu wengi zaidi.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
Tumeshangazwa na kauli ya Ndugu Kajubi Mukajanga (Katibu Mtendaji - Baraza la Habari Tanzania) kwamba CCM haijathibisha kushiriki mdahalo.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
#TaarifaSeptemba23 CCM ilipokea barua ya mwaliko wa mdahalo toka MCT na kuijibu Septemba 13 2015, yenye kumbukumbu namba CMM/OND/M/190/132.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
#TaarifaSeptemba23 Barua hiyo ilisainiwa na Ndugu Stephen Msami (Msaidizi wa Katibu Mkuu CCM), ilipelekwa MCT na ilipokelewa kwa dispatch.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
#TaarifaSeptemba23 Baada ya hapo Katibu Mkuu, Ndugu Abdulrahman Kinana alifanya kikao na wawakilishi wa MCT katika ofisi zetu, Lumumba.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
#TaarifaSeptemba23 Katika Kikao hicho, Katibu Mkuu alitaka kujua zaidi kuhusu mdahalo huo na kutoa maoni kuhusu utaratibu mzima wa mdahalo.

#TaarifaSeptemba23 Ndugu Allan Lawa & Tido Mhando waliiwakilisha MCT katika kikao hicho na Katibu Mkuu - CCM, ofisi ndogo za chama, Lumumba.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
#TaarifaSeptemba23 Katika Kikao hicho, Katibu Mkuu alitaka kujua zaidi kuhusu mdahalo huo na kutoa maoni kuhusu utaratibu mzima wa mdahalo.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
#TaarifaSeptemba23 Jumatano Septemba 16 2015, CCM ilitoa kauli rasmi, iliyosainiwa ikithibitisha ushiriki wake katika mdahalo.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
#TaarifaSeptemba23 Kauli ya Ndugu Mukajanga inalenga kuwasaidia kisiasa wale ambao hawajathibitisha au hawana nia ya kushiriki mdahalo huo.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
#TaarifaSeptemba23 Hivyo tunaamini ni vyema mdahalo huu ukaandaliwa na ushirika wa taasisi mbalimbali zilizokuwa na nia ya kuandaa midahalo.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
Mfano wa taasisi zilizokuwa na nia hiyo ni CEO Roundtable, UDASA & Twaweza. Uandaaji wa pamoja utaondoa ukiritimba katika jambo hili.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
#TaarifaSeptemba23 CCM inasisitiza yafuatayo: 1. Ndugu @MagufuliJP amekubali kushiriki katika mdahalo wa wagombea Urais.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
#TaarifaSeptemba23 CCM inasisitiza: 2. Mdahalo uwashirikishe wagombea wenyewe na sio wawakilishi wao.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
#TaarifaSeptemba23 CCM inasisitiza: 3. Wagombea wote, hasa wa vyama vikuu, wawepo na washiriki katika mdahalo.

CCM haikushangazwa na matokeo ya utafiti wa tasisi huru ya Twaweza ambayo yanatoa ushindi wa 65% kwa Dkt @MagufuliJP kwa sababu kuu 5.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
Wanaohubiri mabadiliko huku wakiogopa kushiriki katika mdahalo wanahubiri mabadiliko hewa.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 23, 2015
1. Siku Ukawa walipomteua Ndugu Lowassa ndio siku CCM ilijihakikishia ushindi. Hatukumteua sababu tuliamini Watanzania wengi hawatamchagua.