Wilaya ya mbinga mkoani Ruvuma imeweka utaratibu wa watendaji wa kata na vijiji kufuatilia mahudhhurio ya wanafunzi shuleni ili kudhibiti utoro kwa wanafunzi na kumpunguzia mzigo mwalimu kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya mbinga Bi.Senyi Ngaga amebainisha hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wakuu wa shule za sekondari kanda ya nyanda za juu kusini uliofanyika mjini mbinga ambapo katika mpango huo watendaji wa kata wanafuatilia mahudhurio ya wanafunzi wa sekondari na watendaji wa vijiji wanafuatilia mahudhurio ya wanafunzi wa shule za msingi.
Kwa upande wao walimu wameiomba serikali kulipa malimbikizo na madai ya walimu na kuborsha mazingira ya shule.
Naye mwenyekiti wa wakuu wa shule za msingi kanda ya nyanda za juu kusini Bw.Ponsiano Ngunguru kupunguza changamoto katika shule za sekondari.