Basi la TASHRIF lapata ajali Tanga, angalia picha zake hapa



Mtu mmoja amekufa papo hapo na wengine wanne wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya TASHRIFF lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dodoma kuligonga gari dogo aina ya Nissan Safari katika eneo la Kange jijini Tanga.


Akizungumza katika eneo la tukio dereva wa gari dogo ANDREW LIMONGA amesema dereva wa basi la TASHRIFF,MOHAMED JUMAA ambaye ndiye pekee aliyefariki dunia katika ajali hiyo hakufunga mkanda.


Amesema basi la TASHRIFF liliigonga gari yale kwa nyuma na alipoyumba akagongwa tena upende wa kulia ndipo magari yote mawili yalipoteza mwelekeo na kuanguka.











JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo