Angalia jinsi mgombea mwenza wa UKAWA alivyopigwa "stop" na wananchi

Msafara wa mgombea mwenza wa chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA ),Mh.Juma Duni Haji uliokuwa unatokea katika kijiji cha Kasanga wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa kuelekea kijiji cha Matayi wilayani humo umezuiliwa kwa zaidi ya nusu saa na wakazi wa kijiji cha kisumba na kusababisha wafuasi wa mgombea ubunge wa jimbo la kalambo kupitia chama cha mapinduzi Josephat Kandege waliovamia eneo la mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa urais,kwa ajili ya kufanya mkutano wao kukimbilia porini ili kuepuka kipigo.

Mapema asubuhi msafara wa Mh.Duni ulipita katika kijiji hicho ukielekea katika kijiji cha Kasanga kilichoko mwambao wa ziwa Tanganyika mpakani mwa Tanzania na zambia ambako mbali na kufanya mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema Mh.Edward Lowassa, mbunge wa jimbo la Kalambo Victor Mateni pamoja na madiwani wa chama hicho – majira ya saa nane mchana ukiwa njiani kuelekea Matayi wananchi wa kijiji cha kisumba waliusimamisha, huku wakimtaka Mh. Duni kuwasalimia lakini jambo la kushangaza katika eneo hilo kulikuwa na maandalizi kwa ajili ya mkutano mwingine wa mgombea ubunge wa CCM ambayo yalikuwa yakiendelea.
 
Alipopanda jukwaani, mgombea mwenza huyo akawapa ahadi wananchi wa kijiji hicho cha kisumba na jimbo la kalambo kwa ujumla, baada ya kujionea mazingira yasiyoridhisha ya utoaji wa huduma za afya katika zahanati ya kasanga na suala la miundombinu ya barabara.
 
Viongozi na makada wa chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA ),akiwemo aliyekuwa mbunge wa viti maalumu chadema mkoa wa manyara Cecilia Paresso pamoja na makamu mwenyekti wa Chadema taifa kutoka zanzibar Said Issa Mohammed wameendelea kuwataka wananchi kupiga kura kwa amani siku ya Oktoba 25 ili kuhakikisha taifa linapata viongozi bora na wenye fikra za kuleta mabadiliko nchini.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo