Watu watano wamekufa hapo hapo na wengine 39
kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Matro walilokuwa
wakisafiria kutoka Rombo kwenda Dar Es Salaam kuacha njia
na kupinduka katika Kijiji cha Manga kata ya Mazingara
wilayani Handeni.
Akithibitisha taarifa hizo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,
Zuberi Mwombeji alisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa
tano asubuhi jana katika kijiji hicho na kudai kuwa bado
wanachunguza chanzo cha ajali ila inaonyesha ilimshinda
dereva na kuacha njia
Kamanda Mwombeji alisema maiti watatu walitambuliwa na wengine wawili hawajatambuliwa
bado na kuongeza kuwa majeruhi walikimbizwa hospitali kwa matibabu
Kamanda Mwombeji alisema dereva wa gari hilo hakuweza kupatikana ametoroka baada ya
kutokea ajali hiyo.