Yule daktari feki aliyekamatwa afariki dunia

Aliyekamatwa kwa tuhuma za kujifanya daktari Desemba 8, mwaka jana katika Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo (Moi), Dismas Macha amefariki dunia katika Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam. 

Mkuu wa Gereza la Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Mbwana Senashida alisema jana kuwa Dismas Macha ambaye Mbwana Senashida alisema jana kuwa Dismas Macha ambaye kesi yake ilikuwa ikiendelea mahakamani, alifariki dunia Agosti 15 mwaka huu kutokana na tatizo la moyo. 

“Alikuwa amelazwa, tulichokifanya ni kuwatafuta ndugu zake na kutoa taarifa polisi,” alisema. 

Senashida alisema mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi jana katika hospitali hiyo, wakati ndugu zake wakisubiriwa kuuchukua kwa ajili ya kuendelea na taratibu za maziko. 

Ndugu wa marehemu ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa maelezo kuwa siyo msemaji wa familia, alisema mwili wa marehemu utasafirishwa leo kwenda mkoani Kilimanjaro kwa maziko. 

“Hili jambo limeshatokea na kwa kweli hatupendi likuzwe maana ngugu yetu ameshatangulia mbele za haki na sisi tunamwachia Mungu. 

Msiba upo Gongo la Mboto,” alisema ndugu huyo. 

Alisema kama ya kugundulika na tatizo la moyo, Macha alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) na alilazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki moja. 

Marehemu Macha alikamatwa baada ya kukutwa akihudumia wagonjwa katika moja ya wodi za Taasisi ya Mifupa (Moi). 

Mkurugenzi Mtendaji wa Moi, Dk Athuman Kiloloma, alithibitisha kukamatwa kwake na kwamba alikutwa akiwa na nyaraka za Moi na vifaa mbalimbali vya kutibu wagonjwa, zikiwamo glovu. 

Alisema vitu vingine alivyokutwa navyo mtuhumiwa huyo aliyefariki ni ripoti za wagonjwa, dawa na vifaa vya kutolea mimba


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo