Kutoka mkoani Njombe: Maisha baada ya Uchaguzi ni matamu zaidi


Na Gabriel Kilamlya Njombe

Waandishi wa Habari Mkoani Njombe Wametakiwa Kutambua Kuwa kuna Maisha Baada ya Mchakato wa Uchaguzi Mkuu Kwa Kuhakikisha Wanachukua Tahadhari Kubwa Katika Kipindi Chote Cha Kampeni Hadi Uchaguzi Mkuu.

Wito Huo Umetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Njombe Bi.Mercy Sekabogo (pichani) Katika Kikao Cha Siku Moja Kilichowakutanisha Wanahabari Ambao ni Wanachama Wa Chama Hicho na Kwamba Umakini na Haki Katika Utoaji Taarifa za Uchaguzi Ndio Utakaomuweka Salama Mwanahabari Yeyote.

Aidha Amesema Kuwa Wanahabari Hawanabudi Kuhakikisha Kazi Zao Haziwezi Kuleta Mpasuko Katika Taifa Kwa Kuandika Habari Zinazoegemea Upande Mmoja wa Kisiasa Jambo Linaloweza Kusababisha Kuwepo na Mpasuko Katika Nchi.

Wakizungumza Mara Baada ya Semina Hiyo Iliyofanyika Katika Ofisi za Chama Hicho Baadhi ya Wanahabari Toka Vyombo Mbalimbali Wamesema Kununuliwa Kwa Baadhi Ya Waandishi wa Habari Kumekuwa Kukisababisha Kushindwa Kutenda Haki Katika Kuripoti Matukio Mbalimbali ya Kisiasa.

Hata Hivyo Wamesema Kupitia Mafunzo Mbalimbali Ambayo Wamekuwa Wakiyapata Wanaamini Kuwa Suala la Kununuliwa na Kuripoti Habari Upande Mmoja Linakwisha Katika Kipindi Hiki Cha Uchaguzi Mkuu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo