Wauawa kwa risasi wakati wakisuluhisha kikao cha wivu wa kimepenzi

Watu wawili wamefariki dunia papo hapo  baada ya kupigwa  risasi katika uwanja wa mpira wa miguu wa shule ya msingi bonye wilayani Morogoro,wakati wa kikao cha usuluhishi kilicholenga kutatua mgogoro wa kimapenzi ulioibuka baina ya mke,mume na aliyetuhumiwa kujihusisha kimapenzi na mke wa mtu,chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Waliopoteza maisha katika tukio hilo lililotokea katika kiwanja cha mpira wa miguu kilichopo  shule ya msingi bonye,kata ya Bwakila chini katika wilaya yà morogoro,ni ally mwinshehe na Said Abdalah ambao walishambuliwa kwa kupigwa risasi wakati wakiwa kwenye kikao ,alichokuwa ameitisha Mwinshehe,kwa nia ya kutafuta suluhu na mume wa Bi.Zena au mama Shakira,Bw.Omary Ngaliwata,baada ya mwanaume huyo kumtuhumu marehemu kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake,aliyeondoka nyumbani baada ya kuibuka tofauti baina yao.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo,amesema  katika kikao hicho kilichofànyika majira ya saa 2 usiku,kikihudhuriwa na watu watano akiwemo mtuhumiwa na mlalamikaji wake,ghafla walitokea watu wengine wawili wakiwa kwenye pikipiki na kuwashambulia kwa risasi,aliyekuwa akilalamikiwa,Ally Mwishee na mwenzake Said Abdala na Mlalakaji Omary Ngaliwata alipora pikipiki yenye namba za usajili  MC 775 AUG  aina ya SUNLG,mali ya Mwishee na kukimbia sambamba na watuhumiwa hao.
 
Kufuatia mauaji hayo,yaliyosababisha watu wawili kutiwa mbaroni wakihusishwa na tukio hilo,akiwemo Haruni Salehe ambaye ni askari w wanyamapori na Athumani Salehe,wananchi wamelaani tabia ya watu kujichukulia sheria mikononi na kutoa wito kwa viongozi wa dini kutoa elimu ya kiroho kwa waumini wao ili kuwa na hofu ya mungu ili kupunguza matukio ya kikatili.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo