"Mchepuko" wa habari waiponza TBC 1, TCRA yaishikisha adabu


Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), imetoa onyo kali kwa Shirika la Utangazaji (TBC1) kwa kuchambua vichwa vya habari vya magazeti kwa upendeleo.
 
Kadhalika Redio ya Magic FM imepewa onyo kali huku ikitakiwa kulipa faini ya Sh milioni 2.5  baada ya kukiuka maadili ya utangazaji kupitia kipindi chake cha 'Morning Magic'.
 
Uamuzi huo ulitolewa jana jijini Dar es Salaam katika mkutano wa waandishi wa habari wakiwemo  wawakilishi kutoka TBC1 na Magic FM, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Wolter Byoga, alisema TBC1 kupitia kipindi chake cha Jambo Tanzania, katika kipengele cha uchambuzi wa magazeti kilikuwa kikiruka habari kubwa na kusoma ndogo.
 
Alisema mtangazaji alikusudia kuruka habari hizo jambo linaloonyesha upendeleo wakati habari ya siku ya Agosti 15, mwaka huu ikiwa moja ya mjadala mkubwa nchini ilitakiwa kusomwa bila ya kuangalia maslahi ya upande mwingine. Aliongeza Gazeti la Nipashe liliandika "Mafuriko Mbeya" ikiwa na picha ya mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema, ilirukwa.
 
Alisema kamati iliangalia kipindi hicho na kubaini kumefanyika ukiukwaji  wa huduma za utangazaji zilizowekwa katika maudhui ya kipindi cha dondoo.
 
Katika utetezi wao ulioandikwa na Mkurugenzi wa TBC, Clement Mshana, alisema kama Shirika hawapangiwi habari za kusoma na pia picha ambazo zilizokuwa kwenye gazeti zilionekana kama za kutengenezwa.
 
Byoga alisema kamati haijaridhishwa na utetezi huo na kusisitiza ukiukwaji wa maudhui ya utangazaji na kuwapa onyo kali na kwamba wakirudia watachukuliwa hatua kali zaidi.
 
Akisoma makosa ya kipindi  kilichokuwa kinaendeshwa na Magic FM, Byoga alisema Julai 16, mwaka huu katika kipengele cha paka rangi, walichambua katuni katika moja ya gazeti na kumtaja jina waziwazi mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli, jambo ambalo ni kinyume na sheria ya utangazaji.
 
Kosa lingine walilifanywa katika kipengele hicho kupitia mtangazaji wake Orest Kawawu, ni kuitafsiri picha hiyo kwa kuihusisha na imani za dhehebu la Katoliki katika kumpata kiongozi wa kanisa hilo ‘Papa’ jambo ambalo linaweza kuleta chuki kwa waumini wa dini hiyo.
 
Watangazaji katika kuendelea kutafsiri katuni hiyo, walisema ule moshi uliochorwa ni mfano wa moshi mweusi unaotoka wakati wa kumtafuta Papa, jambo linaloashiria kwamba aliyependekezwa hafai.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo