Watuhumiwa wa ujambazi wachomwa moto huko Goba

Watu wawili ambao hata hivyo majina yao hayakufahamika mara moja wameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi baada ya kufanya jaribio la wizi katika moja ya duka la Super Maketi katika eneo la Goba jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo limefanyika majira ya asubuhi katika eneo la Goba katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo viajna watatu waliokuwa wakitumia pikipiki aina ya Boxer walipovamia duka moja la Super Makert lililoko eneo hilo na kupora  kiasi cah sh 205, 000 pekee.
 
Licha ya tukio hilo kufanyika hatua chache kutoka kilipo kituo cha polisi, lakini wananchi wanasema katika eneo la Goba kwa muda sasa kumekuwa hakuna usalama wa kutosha kwani matukio ya uvamizi yamekuwa yakitokea mara kwa mara.
 
Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi Kinondoni Kamilius Wambura amesema kumekuwa na operation kali  ya kusaka wahalifu katika eneo hilo ambalo hadi sasa wamekwisha kukamata wahalifu sugu katika eneo hilo wapatao 6.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo