Wanachama wa CHADEMA wavamia ofisi za msimamizi wa uchaguzi Tabora

Wanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA wamefanya vurugu kwenye ofisi ya msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Tabora Kaskazini kutokana na kuwepo wagombea wawili wa chama hicho

Wagombea hao Daudi Nteminyanda aliyeshinda kura za maoni ndani ya chama hicho na Joseph Kidaha aliyepitishwa na chama hicho makao makuu wamekutana katika ofisi za msimamizi wa uchaguzi ambaye alikataa fomu ya Daudi na kuzikubali za Joseph na kusababisha tafrani kwa wanachama wanaomuunga mkono Nteminyanda


Mkurugenzi wa Uchaguzi jimbo la Tabora kaskazini Hadija Makwani amesema kwa mujibu wa sheria zilizopo ofisi yake inamtambua Joseph Kidaha kwa vile ametimiza vigezo na masharti ya kugombea nafasi hiyo


Mgombea ambaye alishinda kwenye kura za maoni Daudi Nteminyanda amesema hakubaliani na maamizi hayo huku katibu wa jimbo hilo Lazaro mayani akisema kuwa yeye amefuata taratibu za chama chake na hajakiuka


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo