Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye ametangaza rasmi hii leo kujiondoa
kwenye chama cha mapinduzi CCM na kujiunga na vyama vinavyounda umoja wa katiba
ya wananchi UKAWA
Sumaye ametangaza uamuzi huo leo katika mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika jijini DSM ambapo amesema anajiunga na UKAWA lakini ni chama kipi
itakujulikana mbele ya safari
Amesema yeye kwenye CCM haondoki ili kukidhoofisha chama hicho, bali anaondoka ili kiimarike, maana yeye anajihisi ni mmoja kati ya makapi yanayotajwa na CCM
Sumaye amesema amefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na uvunjaji wa kununi ndani ya CCM ikiwemo katika harakati za kumteua mgombea wa Urais kwa upande wa CCM akidai mwenyekiti wa chama hicho Jakaya Kikwete alitumia ubabe katika kuwaingiza watu wake tano bora.