Walimu waipa serikali siku 9 tu

Chama cha walimu Tanzania-CWT- kimeipa siku tisa serikali kutekeleza makubalino ya kutatua kero mbalimbali za walimu ikiwemo kulipa deni la zaidi ya shilingi bilioni 19 fedha za mishahara na madai mengine kabla ya kutoa maamuzi kwa wanachama wake.

Akizungumza na waandishi wa habari, rais wa chama cha walimu Tanzania Bwana  Gratian Mukoba ameita kikao dhidi ya serikali kitakachofanyika Agosti 28 kiwe cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa madai ya walimu badala ya mapendekezo, mipango na michakato isiyo na mwisho na kusisitiza CWT hakipendi kuishinikiza serikali kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi bali itambue inawajibu wa kutekeleza makubalino yalifikiwa na CWT.
 
Aidha amesema chama cha CWT kilitegemea serikali kulipa posho ya madaraka kwa walimu wakuu wa shule na wakuu wa vyuo vya ualimu mpaka sasa haijatolewa hali inayotengeneza deni la shilingi bilioni 5 kila mwezi na mwisho wa mwezi huu itaongezeka kufikia bilioni 10, pamoja na walimu zaidi ya elfu 40 wanaostahili kupandishwa daraja kutopandishwa katika mwaka huu wa fedha.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo