Shinyanga kinara wa mimba na ndoa za utotoni

Serikali imeshauriwa kuongeza somo litakalofundisha athari za ndoa na mimba za utotoni katika mitaala ya shule za msingi na sekondari lengo ikiwa ni kuielimisha jamii kuhusu athari zinazowapata wasichana wanaokumbwa na changamoto hiyo hali inayoendelea kurudisha nyuma juhudi za mashirika binafsi za kupambana na janga la umasikini unaowapata wanawake kutokana na kutokua na mwanzo mzuri kielimu.

Hayo yamesemwa na wanaharakati kutoka katika mashirika mbalimbali yanayotetea haki za binadamu wakati wa kuzindua mpango mkakati wa elimu kwa njia ya filamu katika maeneo ya vijijini huku wakiutaja mkoa wa shinyanga kuongoza kwa idadi ya ndoa na mimba za utotoni hali inayochangia kurudisha nyuma jitihada kumkomboa mwanamke kielimu.
 
Aidha baadhi ya wasichana walikumbwa na changamoto ya ndoa na mimba za utotoni wameelezea jinsi walivyoadhirika kisaikolojia na hali hiyo huku wakiitaka serikali kushirikiana na mashirika ya kutetea haki za mtoto wa kike kutoa elimu ya kutosha katika maeneo ya vijijini ili kuikwamua jamii katika dhana ya mila na desturi potofu.
 
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya shinyanga mjini Bi.JoaepHine Matiro amekiri kuwa ndoa na mimba za utotoni ni changamoto kubwa katika mkoa wa shinyanga huku akidai kuwa kuna haja ya kuweka mikakati kati ya serikali na mashirika ya kutetea haki za binadamu kuhakikisha hali hiyo inadhibitiwa kwa kupeleka elimu katika maeneo ya vijijini ili kutokomeza mila na desturi potofu zinazochanigia vifo vya akina mama wajawazito.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo