Kipindupindu sasa ni shiiiiidah....Chahamia mkoani Morogoro, mmoja afariki

Mtu mmoja amefariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu na wengine watatu wamelazwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro ambao kati yao watatu ni familiya moja na mmoja ni familia nyingine.

Mganga mfawidhi wa hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Dr Ritha Lyamuya amesema kuingia kwa ugonjwa wa kipindupindu mkoani hapa nakuwataka wananchi kuchukua tahadhari.
 
Nao baadhi ya wananchi wametoa maoni yao kuhusu ugonjwa huu hatari na wameiomba serikali kutoa elimu kwa wananchi wake pamoja na kutafuta vitendea kazi hasa kwa watu wanaofanya kazi za kuzoa takataka na kuhakikisha mji unasafishwa na kuwa safi ili kujikinga na ugonjwa huo wa hatari. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo