Vurugu kura za maoni CCM, wananchi wakasirika kisa matokeo kucheleweshwa

Viongozi wa chama cha mapinduzi kata ya Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wamejikuta wakifungiwa ndani ya ofisi na wanachama wa chama hicho kwa madai ya kushindwa kutangaza matokeo ya kura za maoni katika nafasi ya udiwani, hali iliyozua vurugu za kurushiana viti na kulazimu viongozi hao kuanza kuhesabu kura upya ili kutenda haki.

blog hii imefika katika ofisi hiyo ya chama kilichopo mtaa wa Madenge tawi la Kisiwani kata ya Buguruni na kukutana na baadhi ya wanachama wa CCM ambao wamesema wanalazimika kulala na kula hapo kwa siku tatu mfululizo wakisubiri kutangaziwa matokeo ya nafasi ya Udiwani bila mafanikio.
 
Baadhi ya wazee na vijana nao wakasema haki haikutendeka katika uchaguzi huo.
Licha ya viongozi hao kufungiwa ndani ambapo ilishuhudiwa kikao kikiendelea huku wakisema kuwa tayari walishatangaza matokeo, hali iliyozua fujo na kurushiana na viti na kulazimu viongozi hao kukiri kuwa wanaanza kuhesabu upya kura.
 
Baada ya vyombo vya habari kuondoka katika eneo hilo, kura zilianza kuhesabiwa upya huku askari wa polisi wakidaiwa kufika katika eneo hilo.

chanzo:ITV

JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo