Vituko vya uchaguzi 2015, Mgombea awapatanisha wake zake jukwaani

Mgombea wa nafasi ya udiwani kupitia Chama cha Wananchi (CUF) na Muunganiko wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Kata ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro mjini hapa, Kondo Mkutu, ametoa kali ya mwaka baada ya kuwaita wake zake wawili jukwaani na kuwapatanisha.

Tukio hilo la kushangaza lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mkutano wa ufunguzi wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Kaloleni ambapo wahudhuriaji walihoji kwamba inawezekanaje mgombea wa siasa kuwapatanisha wake zake katika jukwaa la siasa na wakati sheria za umoja wa nchi zinazounda Jumuiya ya Madola (nchi zilizotawaliwa na Mwingereza), jambo hilo halitakiwi kufanyika jukwaani.

Mkutu anayetarajia kupambana vilivyo na mgombea kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wenslaus Kalogerezi aliamua kufanya hivyo ili kuwaoneshea wapiga kura kwamba kama ameweza kuwapatanisha wake zake wawili, Khadija Enzidoli (mke mkubwa) na Asia Kabwe (mke mdogo) basi hatashindwa kuwapatanisha wananchi wa Mji Mpya na kuwa kitu kimoja.

“Kama hili limewezekana, endapo mtanipa kura zenu katika uchaguzi wa mwaka huu, nitawaunganisha wananchi na kuleta maendeleo,” alisema.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo