Taarifa zaidi kuhusu tuhuma za rushwa kwa Nape Nnauye

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Lindi imemhoji Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa madai ya kukutwa na fedha zinazodaiwa za kuwapa Wajumbe ili wamchague katika kura za maoni.
Nape alikamatwa wakati akitoka ndani ya Benki na alipofika nje alikutana na askari wa kikosi hicho na kumuweka chini ya ulinzi.
Maofisa hao walimchukua kwa mahojiano ofisi ya TAKUKURU yaliyochukua saa tano, kuanzia saa 4:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri na kuachiwa.
Waandishi wa habari waliokuwepo eneo hilo, walishuhudia askari hao wakimkamata na Nape kujaribu kupinga.
Mheshimiwa sisi ni askari wa TAKUKURU , usijivunjie heshima tunakuomba uongozane na sisi kuelekea ofisini kwetu,” alisema mmoja wa askari hao.
Waandishi wa habari walipomhoji Nape kuhusu tuhuma hizo, alikiri kwenda ofisi hizo, lakini alikataa kueleza alichoitiwa na kudai alikwenda kwa ajili ya matembezi yake binafsi.
Mimi sikuhojiwa na Takukuru ila nilikwenda kwa matembezi yangu binafsi,” alisemaNape.
Kamanda wa Taasisi hiyo, Stephen Chami alipotakiwa kuthibitisha tuhuma hizo, aliwataka waandishi wafanye subira kwani wapo katika mahojiano nae, baada saa nne kupita, alipigiwa tena simu na kukiri kumhoji Nape, katika mahojiano hayo Nape alisema fedha hizo alizichukua  kwa ajili ya kuwalipa Mawakala.
Nape ametangaza nia ya kugombea jimbo la Mtama mkoani Lindi ambalo kwa sasa linashikiliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Chanzo: Nipashe


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo