Taarifa ya jeshi la Polisi Mbeya kuhusu mkutano wa Edward Lowassa

Mnamo tarehe 10/08/2015 Ofisi ya Mkuu wa polisi wilaya ya Mbeya ilipokea barua toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inayohusu taarifa ya mkutano wa hadhara utakaofanyika tarehe 14/08/2015 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe. Lengo la mkutano huo ni mgombea wa raisi kuomba wadhamini.


Leo tarehe 13/08/2015 jeshi la polisi mkoa wa Mbeya lilikutana na Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo akiwemo mbunge wa Mbeya Mjini na baadhi ya Madiwani katika eneo la Usalama wa Chama hicho katika ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya na kufanya mazungumzo kisha kufikia makubaliano kama walivyotoa taarifa yao kuwa hakutakuwa na maandamano bali ni mkutano. hii inatokana na sababu za kiusalama pia kutozuia watumiaji wengine wa barabara hiyo ikizingatiwa barabara kuu itakayotumika ni moja. 


Hivyo basi kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya anatoa rai kwa wananchi kutofanya au kulazimisha maandamano yoyote yawe ya miguu au pikipiki. Hii ieleweke kwamba si maandamano bali ni mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja hivyo. Kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.


Imetolewa na: 
Ahmed Z. Msangi – Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo