Tarehe 10 August 2015 katika kipindi cha habari zilizotufikia hivi punde, mtangazaji wetu alisikika akisema jeshi la polisi lapiga marufuku maandamano ya kumsindikiza kuchukua fomu mgombea urais kupitia Chadema.
Katika mahojiano hayo na kamishna Kova aliyekuwa anapinga taarifa za kuzuia maandamano hayo, kwa bahati mbaya wakati wa kuanza na kuhitimisha mahojiano hayo mtangazi wetu alitumia maneno yaliyoleta taswira tofauti.
Uongozi wa ITV unaomba radhi kwa kauli hiyo.
