Rais Dr.Jakaya Kikwete ameliagiza jeshi la polisi nchini kufanya kazi kwa uadilifu ikiwa ni pamoja na kuacha kupokea rushwa ili azma ya kukabiliana na ajali za barabarani zinazoendelea kupoteza maisha ya watanzania iweze kufikiwa.
Rais Kikwete atoa agizo hilo wakati akihutubia mamia ya wananchi, viongozi wa jeshi la polisi, wasafirsihaji na wadau wanaojihusisha na kupiga vita ajali barabarani katika uzinduzi wa wiki ya nedna kwa usalama iliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga iliyobeba ujumbe wa mwaka huu ''Endesha salama okoa maisha''.
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la usalama barabarani nchini Mheshimiwa Pereira Slim amekemea wasafirishaji wanaoendelea kuvunja sheria na kuagiza kuwa sheria haitasita kuchukua mkondo wake kwa yeyote ambaye atakiuka sheria na taratibu zilizowekwa.
