Nimekutana na stori moja kutoka Nigeria ambako Polisi aliyekuwa kazini amekamatwa baada ya picha inayomuonyesha akiwa amelewa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Taarifa hiyo ilisambaa na kumfikia Lagos State Police Commissioner CP Fatai Owoseni baada ya watu wengi kupitia mitandao ya kijamii kuhoji mara mbili mbili uadilifu wa mapolisi hao huku wakidai kitendo hicho kinaleta picha mbaya kwa jamii wanayoizunguka.
Kwa sasa polisi huyo yupo chini ya ulinzi na Police Commissioner ameagiza uchunguzi wa kina dhidi yake ufanyike huku polisi huyo akiwa matatani kufukuzwa kazi ama kupewa adhabu kali.
Polisi Commissioner wa Lagos amesema polisi huyu atakuwa mfano kwa mapolisi wengine amabao hawachukuli kazi zao serious licha ya kuwasihi kutokujihusisha na vitendo vinavyoenda kinyume na sheria zao za kazi ikiwemo sheria inayomzuia polisi kutumia kilevi cha aina yoyote akiwa kazini.
Commissioner wa Polisi Lagos amewashukuru raia wenye matumizi ya mitandao ya kijamii huku akiwasisitiza kuendelea kutoa support zao kwa kuendelea kuwaweka hadharani mapolisi wengine wanaoenda kinyume na wajibu wao wa kiserikali.