Wanaohama CCM kwenda upinzani wapondwa

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chadema, wilaya ya Monduli, mkoani Arusha, Amani Silanga amesema wanachama wanaotoka CCM na kujiunga na vyama vya upinzani ni mamluki na virusi wanaotafuta umaarufu wa kimaslahi.

Silanga ambaye pia alihama Chadema na kuingia CCM ambako aligombea ubunge Monduli, alisema aliyekuwa Mwenyekiti wa chama tawala, mkoa wa Arusha, Onesmo Nangole na aliyekuwa Mwenezi wa Mkoa, Isack Joseph siyo tishio na ndiyo maana waliachia majimbo matatu kwenda upinzani.

Alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha na kusisitiza kuwa hatua ya viongozi hao kuhama chama, haiwezi kukimomonyoa.

Kwa mujibu wake, wanachama waliohamia upinzani, wamemfuata kiongozi wao aliowaweka katika nafasi zao.

“Ningeshangaa sana kusikia mpaka leo Nangole na Joseph wanabaki CCM na kuendelea na madaraka kwa kuwa waliwekwa madarakani na Edward Lowassa (mgombea wa urais Chadema), ’’ alisema na kuongeza: “Hivyo ni lazima wamfuate kila anakokwenda bila ya hata ya kufikiria mara mbili kwa kuwa wanalipa fadhila ya kuingizwa katika siasa.”


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo