PICHA zikionesha nyumba ya Buguruni Malapa iliyoungua leo na kuua watu 9

Familia ya watu tisa imeteketea kwa moto katika tukio la moto uliotokea majira ya saa tisa usiku wa kuamkia leo eneo la Buguruni Malapa Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa majirani, walisikia makelele na walipoamka wakakuta moto mkubwa ukiwa unawaka katika nyumba hiyo hata hivyo juhudi zao za kuvunja mlango ili kuokoa watu waliokuwamo ndani zilishindikana.

Mmoja wa mashuhuda amesema wamefanikiwa kutoa miili ya watu watano iliyoungua vibaya, na imedaiwa kuwa baba mwenye nyumba amenusurika kifo kutokana na kuwa kazini katika shifti ya usiku.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo