Naibu waziri wa nishati na madini CHARLES MWAIJAGE amesema sheria za mafuta na gesi zilizosainiwa na Rais JAKAYA KIKWETE wiki iliyopita zitaleta uelewa katika uendeshaji na udhibiti wa mapato katika sekta ya mafuta na gesi.
Akizungumza kwenye mkutano wa watendaji wakuu wa kampuni za sekta binafsi nchini CEOrt Mwaijage amezitaja sheria hizo kuwa ni sheria ya petroli, sheria ya mapato ya gesi na mafuta na sheria ya madini juu ya uwazi na uwajibikaji.
Akizungumza katika mkutano huo wa CEO roundtable of Tanzania, Mwenyekiti wa CEOrt, ALI MURUFUKI amesema tathmini iliyofanywa na kampuni binafsi inayoonesha kuwa sheria hizo zinamafuu kwa watanzania.
