Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, NEC imefuta Matokeo ya Kura za Maoni ya Jimbo la Singida Mashariki mkoani Singida kutokana na dosari kadhaa zilizojitokeza wakati wa Upigaji Kura.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi NAPE NNAUYE amewaambia Waandishi wa Habari kuwa licha ya uamuzi wa kufuta Matokeo hayo, Jimbo hilo litatakiwa kutangaza nafasi za kugombea Ubunge upya na kwamba Kamati Kuu maalum itakutana tarehe 17 mwezi huu kupitia Matokeo ya Kura hizo za Maoni.
