Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania-TBC, CLEMENT MSHANA
Shirika la utangazaji nchini TBC, limedhamiria kuendelea kuutumikia umma wa watanzania katika tasnia ya habari, elimu na burudani kwa kuzingatia weledi ili kuendeleza amani, umoja na utulivu nchini.
Akizungumzia hatua hiyo katika mahijiano maalumu kabla ya kufanyika kwa mkutano wa siku mbili wa baraza la wafanyakazi wa TBC, Mkurugenzi mkuu wa TBC CLEMENT MSHANA amesema TBC itaendelea kutekeleza majukumu yake ya kuutumukia umma, kwa kuzingatia mabadiliko ya Teknolojia katika habari kwa kuandaa vipindi bora vitakavyoelimisha na kuendeleza amani na mshikamano kwa watanzania.