Mgombea Udiwani wa CCM apigwa risasi

Mgombea Udiwani wa Chama cha Mapinduzi kata ya Sangabuye Mwanza, James Katole amejeruhiwa na risasi na watu wasiofahamika.
Mgomgea huyo alipigwa risasi juzi akiwa kijijini kwake Nyangoka, Busega ambapo alikwenda kuwasalimia wazazi wake.
Katole alisema alikua nje ya nyumba yao majira ya saa 1 usiku akiwa na wazazi wake gafla walikuja watu ambao hawafahamu na alipowahoji ni kina nani hawakuzungumza lolote zaidi kukaa kimya.
‘Walikuwa wamevaa makoti meusi, nilipowauliza shida yao hawakusema loloyte nikaamua kuwafuata ndipo walipofyatua risasi ambayo ilinipata kwenye kidole na kumpiga mama yangu ubavuni na kutokea upande wa pili’ Katole.
Alisema watu hao ambao hawakuchukua kitu chochote baada ya tukio hilo waliondoka huku wakitembea kawadia na kutokomea gizani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo