Mzozo tena ndani ya CCM

Mzozo mkubwa umezuka katika kikao cha wanachama wa chama cha mapinduzi CCM na viongozi CCM kata ya Kimamba “A” kufuatia mgombea wa udiwani aliyeshinda kwenye kura za maoni kukatwa jina na wanachama kulazimishwa kurudia uchaguzi hali iliyosabisha kikao kuvunjika baada ya wajumbe kunyanyuliana viti na kutaka kupigana.

Mwandishi ameshuhudia wanachama hao wakiongea kwa jazba huku wengine wakinyanyua viti kupinga kitendo cha kurudia uchaguzi kwa mara ya pili nakusema endapo watalazimishwa watakihama chama hicho na kwenda vyama vya upinzani ambapo kikao kilivunjika na wajumbe wakaanza mzozo na mambo yalikuwa hivi.
 
Aidha wanachama hao wameitaka viongozi CCM wilaya kutovuruga matokeo hayo na kumtangaza aliyeshinda na vinginevyo wachague mwingine kati ya watu watano waliogombea huku mwenyekiti wa kata Mussa Guzungwa ambae ndiye aliyeshinda kura za maoni kugombea udiwani akijiuzulu na kuhamia vyama vya upinzani.
 
Naye katibu wa CCM kata ya Kimamba “A” Samweli Warioba amesema tarifa hizo za malalamiko ya wanachama wamezipeleka kwa viongozi wa CCM wilaya ya Kilosa na kwamba hawakubaliana na maamuzi ya kurudia uchaguzi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo