Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dkt Regnald Mengi ametangaza zawadi kwa vijana wote wa kitanzania waliozaliwa mwaka 1994 wakati gazeti la Nipashe lilipoanza kuchapishwa nchini.
Dkt Regnald Mengi ambaye pia ni mwenyekiti wa makampuni ya IPP, ametangaza zawadi hiyo jijini Dar es Salaam ikiwa ni katika maadhimisho ya kusheherekea gazeti la Nipashe kutimiza miaka 21 sokoni.
Kwa uapnde wake mhariri mtendaji wa gazeti la Nipashe Bw Jesse Kwayu amesema kumekuwa na mafanikio makubwa tangu gazeti hilo linalotamba kwa habari za uhakika lianzishe.
Aidha ametumia fursa hiyo kusisitiza kuwa wataendelea kusimamia ukweli na kamwe gazeti la Nipashe halitatumika katika kuunga mkono chama chochote cha kisiasa hasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Gazeti la Nipashe lililokuwa kwenye muonekano mpya lilionekana kupendwa zaidi katika siku yake ya kwanza kama ambavyo Bw John Magesa muuzaji wa magazeti anavyozungumza.