Mkuu wa wilaya matatani kwa kudaiwa kupora kiwanja cha mjane

Mkuu wa wilaya ya muleba mkoani kagera,Francis Isaac,amepandishwa kizimbani, mbele ya baraza la ardhi na nyumba, wilaya ya Singida, akidaiwa kupora kiwanja cha mjane mmoja, kilichopo katika mtaa wa minga, manispaa ya Singida.

Issac ambaye aligombea ubunge,jimbo la mkalama,mkoani Singida na kuambulia nafasi ya tatu wakati wa zoezi la kura za maoni Agosti Mosi mwaka huu, katika madai hayo, ameunganishwa na shekhe mmoja aliyetajwa kwa jina la Salumu Rajabu Sima.
 
Mbele ya baraza hilo, mwenyekiti Saidi Wambili amesema kuwa, juni 15, 2012, mlalamikiwa isaac kwa kushirikiana na Shekhe Sima, walikula njama ya kuchukua kiwanja namba 116,kitalu ‘s’, mali ya Amina Abdallah (80), bila ya kibali chochote kisheria.
 
Katika hati yake ya madai, amina ambaye ni msimamizi wa mirathi ya marehemu mumewe, Kilawe Nchomba, analitaka baraza hilo liwaamuru walalamikiwa hao, kumlipa sh.milioni nane, ikiwa ni fidia ya kubomoa jengo lililokuwemo awali, kwenye kiwanja hicho.
 
Amina pia ameliomba baraza hilo liwazuie walalamikiwa hao kuingia ndani ya kiwanja hicho, waache kukiendeleza na baraza limtangaze yeye (amina) kuwa ndiye mmiliki halali wa eneo hilo.
 
Mapema akitoa ushahidi,Ofisa ardhi manispaa ya Singida,Gaudence Mwakalomba amesema ,awali kiwanja hicho kilimilikiwa na Kilawe nchomba,lakini baadaye sima alikihamisha kinyemela hadi kwa Francis Isaac,bila ya kufuata taratibu.

Hata hivyo shauri hilo namba 32 la mwaka 2013,linasikilizwa na baraza bila ya walalamikiwa kuwepo,kutokana na kupuuza amri ya baraza hilo kuwataka wahudhurie limeahirishwa.
 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo